CRDB Wakala ni wakala wa kibenki waliopitishwa na kufundishwa utoaji huduma za kifedha kwa niaba ya Benki ya CRDB kulingana na kanuni na mwongozo wa Benki kuu ya Tanzania.
Faida za kuwa CRDB Wakala;
- Kufanya biashara na Taasisi kubwa inayoongoza kwa utoaji huduma za kifedha Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla.
- Kupata malipo mazuri kutokana na kutoa huduma kwa wateja wakubwa wa CRDB.
- Ongezeko la wigo wa wateja katika biashara yako.
- Kuleta ufanisi katika biashara yako kwa usimamizi wa pesa.
- Kuongeza uwezo kupitia mafunzo ya bure kutoka Benki ya CRDB katika masuala ya kijasiriamali, huduma za kibenki, na mbinu mbalimbali za kuzuia utakatishaji fedha na udanganyifu wa kifedha.