Yajayo hayatabiriki

Pata Bima ya maisha inayokupa akiba kwaajili yako na wale uwapendao

Jipange

Pata Bima 

Bima ya Maisha

Ni Bima yenye faida ya kuweka akiba kwa malengo ya baadae. Ni Bima maalum kwa mipango endelevu kama Elimu kwa faida yako na wale uwapendao. Pia inakupa uhakika pale majanga yanapotokea na kufanikisha malengo yako uliyoyapanga kwa muda maalum ulioweka.

Sifa;

 • Bima hii ina sehemu ya kupata fao la bima ya maisha na mpango wa kuweka akiba
 • Fao la Bima ya Maisha ni kuanzia Tsh 3,500,000 mpaka Tsh 50,000,000
 • Umri wa kujiunga kuwa na Bima hii ni kuanzia miaka 18 mpaka miaka 60 
 • Mkataba wa mpango huu wa Bima unapaswa kuwa kati ya miaka 7 hadi miaka 18
 • Kiwango cha chini cha akiba kwa mwezi ni Tsh 7,500 na hakuna kikomo cha kiwango cha juu
 • Malipo yanapaswa kufanywa ndai ya siku 30 baada ya mpango kumalizika
 • Wanufaika wa Bima watapata faida mara mbili endapo kifo cha mteja kitasababishwa na ajali (Double indemnity)
 • Kwa kifo ambacho hakijasababishwa na ajali malipo yake yatasubiri kwa muda wa miezi sita
 • Mnufaika anaweza kuwa mtu yoyote anayeaminika na mteja
 • Endapo atakosekana mnufaika wa fao la akiba aliyelengwa, nafasi yake inaweza kuchukuliwa na mnufaika mwingine
 • Malipo yanaweza kufanyika kwa pesa taslim au kwa malipo yanayojirudia kwa kutumia njia yoyote kupitia akaunti ya Bima

Faida;

 • Bima ya Maisha; Ikitokea mwenye Bima amefariki, fao la maisha litalipwa kwa mkupuo kuanzia Tsh 3,500,00 hadi Tsh 50,000,000. Pia fao la akiba litalipwa lote mara moja kama mwenye bima hajaweka kinga ya kusamehe michango. Endapo mteja ataweka bima ya akiba (WOP) , fao lake la akiba litaendelea kulipwa kama mkataba unavyosema.
 • Faida ya kuweka akiba; Ukifika ukomo wa muda uliopanga kuweka akiba, akiba yako yote italipwa pamoja na riba iliyojumuishwa kwa kipindi chote.  
 • Kutoa pesa; Unaweza kutoa pesa ndani ya kipindi cha makubaliano lakini hutoruhusiwa kutoa pesa zaidi ya (nusu) 50% ya akiba iliyopo.
 • Ikitokea umefariki au umepata ulemamavu wa kudumu kampuni ya bima itaendelea kulipa michango kwa niaba yako kwa kiasi sawa na michango ya akiba ambayo ulikuwa ukilipa kabla ya kifo au ulemavu
 • Unaruhusiwa kukatiza mpango wako wa bima kabla ya kufika ukomo wa muda uliopanga
 • Unaruhusiwa kuendelea kukuza kiasi cha pesa ambacho tayari kipo kwenye mpango wako wa akiba au bima ya maisha endapo utashindwa kuendelea kuweka akiba au michango ya fao la maisha
 • Faida ya kulipwa pesa taslim; Lengo la kulipwa pesa taslim ni kurudisha jumla ya akiba yote uliyoweka ndani ya kipindi cha makubaliano
 • Lipo fao la likizo la kutolipa michango hadi mwaka mmoja kwa mwenye bima aliye mjamzito au atakayepoteza ajira akiwa ndani ya mpango wa bima.
 • Malipo ya bima ya maisha au akiba yanaweza kufanyika kwa utaratibu mmoja wapo yaani kila mwezi, kila robo mwaka, kila nusu mwaka au mara moja kwa mwaka.

 

Madai;

Unaweza kulipwa mafao yako ya akiba kama upo hai na endapo ikitokea hautakua hai watalipwa wategemezi wako.

Taratibu za kulipwa ni kama ifuatavyo;

 • Tupe taarifa juu ya madai yako kwa njia ya barua pepe info@crdbbank.com au tembelea tawi lolote la CRDB.  
 • Jaza fomu ya madai utakayopewa kisha iwasilishe.
 • Wasilisha viambatanisho vyako kama kitambulisho, hati ya makubaliano ambavyo vitakusaidia kudai akiba yako  

Pata Bima